Sunday, October 2, 2016
SIMBA WAONYESHA UBABE MBELE YA WAPINZANI WAO WA JADI YANGA, BAADA YA KUSAWAZISHA BAO HALI YA KUWA WAPO PUNGUFU.
Simba walicheza pungufu uwanjani baada ya mchezaji wao muhimu kabisa JONAS MKUDE kutolewa nje na muamuzi wa mchezo kwa kadi nyekundu, Lakini vijana hao wa wekundu wa msimbazi hawakukata tamaa ya kuendelea kusakata kabumbu japokuwa walikuwa tayari wapo nyuma kwa bao moja kwa bila,bao lililofungwa na HAMIS TAMBWE kwa upande wa yanga, Simba walionyesha kiwango cha hali ya juu uwanjani baada ya kurudi kipindi cha pili na mnamo dakika cha majeruhi Simba walipata bao maridadi kabisa kutoka kwa kiungo wao mshambuliaji SHIZA RAMADHANI KICHUYA baada ya kupiga kona ya moja kwa moja na mpira kuzama wavuni..Mchezo huo umemaliza kwa sare ya 1 - 1 na Simba wakiendelea kuongoza ligi kuu kwa kubaki kileleni kwa pointi 17 mkononi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment