Sunday, October 2, 2016

MOURINHO AANZA KUJITETEA MANCHESTER UNITED.

Jose Mourinho amesema anahitaji kupewa muda zaidi ili kuitengeneza Manchester United na kuwa bora.

United wanakabiliwa na kibarua kigumu mbele ya Stock City katika Uwanja wa Old Trafford Jumapili hii kabla ya kwenda mapumzikoni kupisha mechi za kimataifa na baadaye kurudi kukabiliana na Liverpool, Fenerbahce, Chelsea na Manchester City michezo hiyo ikichezwa ndani ya siku tisa
Na sasa akiwa tayari ameiongoza United kwenye michezo 10 tu, Mourinho amesema hatarajii kuwa amewajua kwa undani wachezaji wake pengine mpaka akae nao muda mrefu zaidi.
“Nahitaji muda, Nahitaji kuona wachezaji wangu wanacheza, Nahitaji kuwaona wakiwa na utofauti mkubwa, Nahitaji kuwafahamu zaidi,” Mourinho aliwaambia wanahabari.
“Kuna mambo mengi sana ya kuangalia ili niwasome wachezaji wangu vizuri na hayo yote yatawezekna endapo nitakaa nao muda mrefu. Mara nyingi kuna utofauti kidogo unapokuwa umekaa na timu kwa miezi mitatu au minne na pengine mitano.”

No comments:

Post a Comment