Majina ya wasanii watakaowania tuzo za MTV MAMA 2016 yalitajwa huku Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz na kundi la Navy Kenzo ndio wasanii wa Tanzania waliotajwa kuwania tuzo kubwa za Africa za MTV Africa Music Awards 2016. Navy kenzo waeleza furaha yao baada ya kutajwa kuwania kipengele cha kundi bora la mwaka kwenye tuzo hizo.
"Tunashukuru sana tumepata taarifa za MTV MAMA 2016 tumechaguliwa kwenye Best Group yaani tumefurahia sana ni kitu ambacho kimetutia nguvu sana
Kimeonesha jinsi gani kazi yetu ambayo tuliyokuwa tukifanya kwa muda mrefu ndio imeanza kuleta matunda hayo kwahiyo tunashukuru sana, tutatoa maelekezo katika mitandao yetu ili mashabiki wetu na wengineo wajue jinsi ya kutupigia kura"
No comments:
Post a Comment