Cristiano Ronaldo amepiga chini dhana ya uadui uliyopo baina yake na Lionel Messi na kusisitiza kuwa wawili hao wanaheshimiana, licha kuwa hawana urafiki wa aina yoyote
Staa huyo wa Real Madrid na mwenzake wa Barcelona wamekuwa wakitawala tuzo ya Ballon d’Or kwa takriban miaka nane mfululizo na kupelekea dunia ione kwamba wao ndio wachezaji bora kabisa duniani kwa sasa.
Kuna mjadala mkubwa sana miongoni mwa watu kuhusu nani bora kuliko mwingine, lakini Ronaldo amekataa kueleza kuwa nani mkali zaidi ya mwenzake.
“Mimi na Messi tunaheshimiana sana,” Ronaldo alinukuliwa na jarida la Coach Magazine.
“Vyombo vya habari vinapenda sana kukuza na kueleza kwamba kuna uhasama mkubwa kati yetu, lakini si kweli.
“Si kana kwamba kuna urafiki mkubwa kati yetu,lakini tunaheshimiana sana,” Alisema Cristiano Ronaldo.
No comments:
Post a Comment