Sunday, October 30, 2016

MOJA KATI YA BEEF KUBWA LILILOKUWEPO KWENYE MUZIKI WA AFRIKA LIMEKWISHA, CASSPER NYOVEST NA AKA SASA AMANI IPO

Bifu hiyo imeisha baada ya AKA kwenda kumpongeza hasimu wake Cassper kwenye show yake ya kihistoria Jumamosi, iliyomshuhudia akiweka historia kubwa ya kuwa msanii wa kwanza wa hip hop kutoka nchini humo kuujaza uwanja wa mpira wa Orlando jijini Johannesburg
Baada ya show hiyo, AKA alimfuata Cassper na kumpongeza kwa hug zito. Picha za wawili hao wakiwa wamekumbatiana zimekuwa gumzo mtandaoni huku baadhi ya mastaa wa nchini humu wakiwapongeza kwa kumaliza uadui wao.
Hata kabla ya show hiyo, AKA aliandika kwenye Twitter: Good Morning! This is the day the lord has made. @casspernyovest, today is your day. Good luck & God bless.
Cassper alijibu: Thanks for the well wishes. God bless
Na hata girlfriend wake na AKA, Bonang Matheba alikuwa na moyo huo huo kwa kuandika kwenye Twitter: All the best tonight @CassperNyovest… God is good. All the time… Your dream will come true. The country supports you.


No comments:

Post a Comment