Friday, October 21, 2016

ORODHA MPYA YA FIFA YA TIMU BORA ZAIDI DUNIANI.


fifa

Shirikisho la soka duniani (FIFA) imetoa orodha mpya ya viwango vya ubora wa soka duniani, bado vinara wamesalia kuwa Argentina

Mabadiliko haya yamekuja hasa kwa kuzingatia Matokeo ya Mechi za kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Urusi.
Tanzania inashika Nafasi ya 144 baada ya kuporomoka nafasi 12. Uganda wao wapo nambari 72 baada ya kushuka nafasi saba, Kenya wamepanda nafasi sita hadi nambari 85 nao Rwanda wamesalia nambari 107.
Ethiopia wamo nafasi ya 126, Malawi 100 na Burundi 138.
Nchi ambayo ipo juu kabisa kwa Bara la Afrika ni Mabingwa wa Afrika Ivory Coast walio nafasi ya 31 wakifuatiwa na Senegal ambao ni wa 32.
Orodha nyingine ya Ubora wa viwango itatolewa Novemba 24.
Haya ni mataifa 10 bora duniani
1.Argentina
2.Ujerumani
3.Brazil
4.Ubelgiji
5.Colombia
6.Chile
7.Ufaransa
8.Ureno
9.Uruguay
10.Uhispania
Mataifa 10 bora Afrika
31 Ivory Coast
32 Senegal
35 Algeria
38 Tunisia
45 Ghana
46 Misri
49 DR Congo
58 Mali


59 Cameroon

No comments:

Post a Comment