Baada ya kudumu kwa zaidi ya miaka minne, bifu la Patrice Evra na Luis Suarez sasa limefika tamati. Evra amempongeza Suarez baada ya kukabidhiwa kiatu cha dhahabu (European Golden Shoe) kwa kuibuka mfungaji bora barani Ulaya msimu wa mwaka 2015/2016
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Evra ameandika, “ kuna neno upendo tu na hakuna neno chuki !!! Luis, wewe ni mchezaji mkubwa na bora sana, wewe ni namba tisa bora, hongera sana Luis @ luissuarez9. Naupenda sana huu mchezo !!! hahahaah.”
Ugomvi wao ulianza mwaka 2011 wakati wa mechi yao iliyochezwa kwenye uwanja wa Anfield ambapo Evra alidai Suarez alimkashfu kwa maneno ya kibaguzi kitendo ambacho kilisababisha FA kumuadhibu mchezaji huyo kutocheza mechi nane na kulipa faini ya £40,000.
Wachezaji hao walithibitisha kuwa ugomvi wao haushikiki mwaka 2012 wakati wa mechi yao iliyochezwa kwenye uwanja wa Old Traford ambapo Suarez aligoma kumpatia mkono Evra.
No comments:
Post a Comment